Mmh, mmh
Oh yeah yeah yeah yeah yeah yeah

Mbio za sakafuni huishia ukingoni sikujua
We nenda salama mi najiuguza
Wameshakurubuni fadhila zangu huzioni natambua
Siwezi kung'ang'ana ushanipunguza

Hee ninajihisi bahati sina, sahau yote ya jana
Bora ungesema mapema kama kuna kosa nilokutendea
Uliniahidi utanilindia heshima, hutaifanya danga
Kumbe hata yale maneno mazuri uliyosema uliongopea

Ooh Baba! Kumbe siri ya mtungi aijuaye kata
Ooh Baba! Moyo umeumbwa kupenda mwingine nitapata
Ooh Baba! Yakiisha mavumbi mafua yatakata
Ooh Baba! Na ukweli haufungwi kwenye penzi la balaa

Sina bahati, sina bahati
Sina bahati, sina bahati
Nilishajaribu kufosi hadi kupiga ndele (sina bahati)
Ila bado nimikosi acha niende mbele

Eh sishindani na upepo kwa mbio
Limenikosa sikio
Mie kichwa nijigeuze kalio
Bure nitajiumiza
Mizani haipimi kulia
Shetani amelibamia
Siku hizi anajiita fagio
Anawamaliza eeh

Mwili wema wangu umeniponza
Ni mifupa nono kulifyonza
Umeniacha njia panda mi naoza
Bila huruma
Masikini moyo umenichonza
Jahazi lazama ye nahodha
Mateso kila likichomoza
I wish siku zirudi nyuma

Ooh Baba! Kumbe siri ya mtungi aijuaye kata
Ooh Baba! Moyo umeumbwa kupenda mwingine nitapata
Ooh Baba! Yakiisha mavumbi mafua yatakata
Ooh Baba! Na ukweli haufungwi kwenye penzi la balaa

Sina bahati, sina bahati
Sina bahati, sina bahati
Nilishajaribu kufosi hadi kupiga ndele (sina bahati)
Ila bado nimikosi acha niende mbele
    Página 1 / 1

    Letras y título
    Acordes y artista

    restablecer los ajustes
    OK