This is AY from Tanzania Maurice Kirya and MD from Uganda It’s a dedication to all Africans living in poverty Yeah! Usiombee mambo yaharibike Pesa usiishike mfano wa mti upukutike Utaonekana si lolote, si chochote Utaonekana karaha kwa watu siku zote Walimwengu hawatakupa mkono Magonjwa yatakuvuta ndani ya shimo Utakata tamaa, utaandamwa na balaa Pumzi hutoivuta kwa raha Kweli usiombe ikuwai Survive for fittest, never trust nobody this world of weakness Watakukana hata kama ndugu zako Watadiriki sema hawajui utokako Mama acha kulia, hali ulio nayo ni majaribu tu ya dunia Ipo siku mambo yako yatatulia Utaweza hata kusahau ya zamani uliopitia Oh hii dunia! Baga lalinaa aah Gendo okore You should think about tomorrow, not only today Baga lalinaa aah, gendo okore Oo uuh, gendo okore Wapo wapi marafiki ulokuwa nao Enzi zile pesa imekutembelea? Hawapo tena nawe wamekukimbia Sasa uko waliko tayari wanakukandia Mke wako nae anataka taraka Anasema maisha nawe ameshachoka Anataka arudi kule kwao alipotoka Sababu maisha anayoishi nawe ameshachoka Ada ya watoto hujalipia Kodi ya chumba nayo unadaiwa Unazidi changanyikiwa hata unajuta oh kwanini ulizaliwa Piga moyo konde, maisha uyashinde Bado safari ndefu yenye miba na mabonde Usiweke kinyongo hata kama alikutupa Remain strong, these tryna be jealous That’s all! Baga lalinaa aah Gendo okore You should think about tomorrow, not only today Baga lalinaa aah, gendo okore Oo uuh, gendo okore Binadamu sio watu Ukiwa na shida hutowaona Ona sasa wamekimbia, uuh oh Ona sasa wamekimbia! Binadamu sio watu Ukiwa na shida hutowaona Ona sasa wamekimbia, uuh oh Ona sasa wamekimbia! Baga lalinaa aah Gendo okore You should think about tomorrow, not only today Baga lalinaa aah, gendo okore Oo uuh, gendo okore (Ni kweli watakupenda ukiwa na kitu tu) Ukiwa na shida hutowaona (Watakujali vipi ukiwa na shida ndugu yangu?!) Ona sasa wamekimbia, uuh oh (Kali, Rasheed) Ona sasa wamekimbia! (ECT, Master Jay) Ona sasa wamekimbia! (Maisha yana pande mbili, usife moyo) Ona sasa wamekimbia! (Zingatia, sikia, siku zote ndo yanavyotokea)