Wee nipende hivyo hivyo mamaa
Japo mambo ndivyo sivyo mamaa
Punguza na masikitiko sanaaa
Tupendane mpaka kifo mamaa

Aah eeh, aah eeh
Aaah eeh, mama oohh
Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, mama oohh

Jana tumelala njaa
Paka amelala jikoni
Kibanda chetu chavujaa
Usiku tunalala kihunii

Ulisema utanipenda mpaka mwisho
Hutonikimbiaa yaaah
Na hali yangu ni ngumu mahangaiko
Utavumilia yaah

Aah eeh, aah eeh
Aaah eeh, mama oohh
Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, mama oohh

Mbona nayona mengi natamani
Lakini natuliza moyooo
Japo wanasema mengi majirani
Napuuza naachana nayooo

Mwenye nacho anaongezewa (eeh)
Urefu wa kamba nasubiria (eh)
Bila Imani utanikimbia mpenzi (eeh)
Kwa hii hali nachechemea (eh)

Shilingi yaua mume wangu
Mlinzi nalinda pendo langu
Japo kidogp ndo cha kwangu
Mungu anajua kesho yangu

Aah eeh, aah eeh
Aaah eeh, baba oohh
Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, baba oohh

Nakupenda hivyo hivyo baba
Japa mambo ndivyo sivyo baba
Hata na mahangaiko hayaaa
Ntakupenda mpaka kifo baba

Aah eeh, aah eeh
Aaah eeh, baba oohh
Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, baba oohh

Kazi nimefukuzwa
Kibarua kimeota nyasi mamaa
Joto lanifukuta
Mfukoni sina hata hela ya ngama
Nasikia mama mwenye nyumba nae
Anataka kodi yake, hivi kweli
Mazonge yamepitilza
Na sipati jibu lake saa nafeli

Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, mama oohh
Aah eeh, aah eeh
Aah eeh, mama oohh

Piga konde baba
Kidogo ndo ujaza kibabaa
Ridhiki mafungu saba
Tunachopata tushukuru si haba
Ukweli kusema nakupenda tu
Sijari kwa hali iwe chini ama juu
Wao kwa magari sisi kwa miguu
Tule kachumbali miguu ya kuku (huu huu)

Mkono mtupu haulambwi baby
Utanipenda vipi
Penzi tupu bila pesa halitambi
Utanielewa vipi

Nimeamini kweli wee kipenda roho
Na nyama mbichi imenikaba koo
Tule kipolo (aah eh)
Giza totoro (yaa wee)

Uuh mama yee (mmh)
Wee chaguo langu

Wee baba we
Wewe mwandani wangu

Nitakupenda milele

Unipende milele
Nitakupenda milele
Iyee iyee iyee...

Aah eehh
Aah eeeh
Uuhh
Uuhh
Ayee he
    Página 1 / 1

    Letras y título
    Acordes y artista

    restablecer los ajustes
    OK