Mama ananambia Naseeb Mi ni mtu mzma nawe ndo nakutegemea Yanayotokea jaribu kupiga kimya usidiriki ata kuongea Mara nasikia vya aibu Konda, Gwajima eti ugomvi umekolea Kuchunguza karibu ni binti mmoja kwa mitandao wanachochea Najaribu kunyamaza, ila moyo hautakii Unanambia eti Simba japo unguruma uisemee hakii Ooh najaribu kunyamaza ata Laizer ataki yoo Anasema walau nena kidogo (hiih) Na mashabiki Dangote Wananambia mbona husemi chochote, ah Si uko nao siku zote Ama ulezi unafanya uogope, ah Na media pande zote Wanalalama kiongozi atoke eh Nchi inaingia matope Niende wapi na mi mtoto wa wote Yaani lawama Wacha nikae kimya Mmh nisiongee (kimya) Ooh ninyamaze mimi (nikae kimya) Nisiseme (kimya) Mama kanambia (wacha nikae kimya) Ooh nifunge mudomo (kimya) Mie bado mdogo sana (nikae kimya) Nisiseme (kimya) Mmh ni mengi majaribu Najatahidi epuka yasije nicost Japo mengine swadakta mengine hayana maana Rafiki kipenzi wa karibu Hata nyimbo yake sikuweza ipost Ila alivokamatwa iliniumiza sana Mitandaondi kila kona Uongo na ukweli unashonwa Kila nyumba inanong'ona Ah oh Tanzania Mara kimbembe Dodoma Bunge upinzani wamegoma Juzi akapotea na Roma Oh Tanzania, ooh Najaribu kunyamaza, Makame hataki yooh Ananambia walau nena kidogo Nyumbani nafungua gate Niende kwa Mangi nunua super gate eh Napewa za chini ya kapeti Kuna redio imevamiwa kefti eh Napita kwenye (magazeti) Nakuta rundo la watu (wameketi) Eh, badala ya kutafuta cent Wanabishana tu mambo ya vyeti Wacha nikae kimya Ooh nisiongee (kimya) Ninyamaze kabisa (nikae kimya) Eh ulimi koma (kimya) Usije kunipoonza (acha nikae kimya) Nifunge bakulu lanhu (kimya) Nikojoe nikalale (nikae kimya) Mi bado mdogo sana (kimya) Mama kanambia Oh najiuliza (waapi) Najiulii (waapi) Tunakwenda wapi (waapi) Kila siku maneno (waa) Ah tuacheni jamani (waapi) Mi na we ni taifa moja (waapi) Kambarage baba mmoja (waa) Sa tofauti za nini tushikamane Tukaijenge Tanzania