Ay-Ayo, Trone Mmh Ni utoto tu, ila mie kwako sipindui Ndio maana usiku nikinuna, najichekesha asubuhi Ni ujinga tu, ila mie kwako fala Ndio maana usipo pokea simu, siwezagi lala Mm, umenifunza tofauti ya kupenda na kupendana Na kuongea sio sauti hata macho husemezana Na mapenzi yanataka, 'imara, kuaminiana Nami kwako sina shaka, 'ewawa, utachofanya Na hivi vi inzi, vya kuzengea wizi Vikija anga hizi, visikunyime amani Lala usingizi, upepo barizi Mie mambo ya uzinzi, 'aku vya kazi gani, baby? Hapo hapo ilipo mbao (gongelea na msumari) Oh, penzi letu tuboreshe (gongelea na msumari) Ezeka na bati, honey (gongelea na msumari) Mvua ya chuki isipenyeshwe (gongelea na msumari) Mm, mm-m Oh, njiwa nenda, njiwa, 'njiwa peleka salamu (peleka salamu) Naivasha, Kivule, 'Mombasa zifike Lamu Njiwa nenda, njiwa, 'njiwa peleka salamu Ziende mpaka kwa yule, 'lonitesa mwanaharamu Si alisema mimi, sitopata wa thamani Asa hii ni nini? Umuulize huyu nani Wamebaki kutabiri si punde tutaachana Wambie sio kwa penzi hili, mbona wataroga sana Na hivi vi inzi, vya kuzengea wizi Vikija anga hizi, visikunyime amani Lala usingizi wewe, upepo barizi Mie mambo ya uzinzi, 'aku vya kazi gani, baby? Hapo hapo ilipo mbao (gongelea na msumari) Oh, penzi letu tuboreshe, darling (gongelea na msumari) Ezeka na bati, honey, oh (gongelea na msumari) Mvua ya chuki isipenyeshwe (gongelea na msumari) Mm Wasafi