Mja hapati, hapati alitakalo Bali hupata, ajaliwalo na Mungu Usikonde, kwa hili nilipatalo Hilo ndilo, hilo ndilo langu fuu Mja hapati, hapati alitakalo Bali hupata, ajaliwalo na Mungu Usikonde, kwa hili nilipatalo Hilo ndilo, hilo ndilo langu fuu Sudi, sudi sudini Bahati ya mwenzio, usilale mlango wazi Sudi, sudi sudini Bahati ya mwenzio, usilale mlango wazi Ni lipi nililowakosea? Mbona yenyu ni machafu hamsemi Mabaya, kutwa kunipakazia Kama nina deni niambieni Maana kila siku maneno Mie si mtu, hilo linatoka wapi? Mmenibadilisha jina naitwa mchawi Tena hasidi, yote yanatoka wapi Maana kila siku maneno Mie si mtu, hilo linatoka wapi? Mmenibadilisha jina naitwa mchawi Tena hasidi, yote yanatoka wapi? Niliyajua mapema ndo maana nikapuuzia Washa zoea kusengenya ndo maana nawapotezeaga Si hofii mi wenu unafiki, shingoni sijitii kamba Wajidanganya na vyenyu visiki, sumu yenyu sitoilamba Alopewa na Mola hapokonyeki, wala msijisumbuke kwa dumba Wajidanganya na vyenyu visiki, sumu yenyu sitoilamba Mwanitangazia, mwajitangaza mitaani Kwamba mnanijua, mimi kiundani wewe Kuliko hata alonileta duniani wewe Tena mnajinadi, huko mitaani wewe Kwamba mnanijua, mimi kiundani wewe Kuliko hata alonileta duniani wewe Nyie kama mahodari basi naye mseme Yaani nyie kibindoni wana wa wezenu midomoni Nyie kama mahodari basi naye mseme Yaani nyie kibindoni wana wa wezenu midomoni Sudi sudini, asiye bahati habahatishi Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi Mwajipatia dhambi nyinyi, nalala mie sikeshi Ikiwa kuna kuozwa nahisi nimetenda Basi niko radhi chini niweke mimi Kuliko kukaa pembeni, mabaya kuzua Na mimi nina roho, kama nyinyi Hata ukiwa mwerevu wao watakugeuza ng'ombe Kusudi wakupake majivu, hao hawana aibu viumbe Nafeli kwa kukosa usikivu, hamna subira hata chembe Mnapoteza mwenzenu kwa mambo yenu ya kizembee Sibabaiki na yenu majungu mie Mie nawaua kisugu mie Mwasaka kiti kupitia jina langu Ukimya ndo sina haya hangu mie Mmesahau kuwa kuna Mungu Mwapinga ramli chini ya uvungu nyie Sudi sudini, asiye bahati habahatishi Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi Mwajipatia dhambi nyinyi, nalala mie sikeshi Sudi sudini, asiye bahati habahatishi Sudi nichukie nyinyi, tamaa hamnikatishi Mwajipatia dhambi bure, nalala mie sikeshi Pole, pole sana eeh Pole, pole sana eeh Na kila kitu mimi Mimi mchawi wako mimi Mimi hasidi yako mimi Mimi na ubaya wako mimi Kila kitu mimi Pole, pole sana eeh Pole, pole sana eeh Umeshinda ugangani, kesha uchawini Sina hirizi shingoni, shina ushale mwilini Mimi najiamini, namtegemea maanani Pole, pole sana eeh Pole, pole sana eeh Na kila kitu mimi Mimi mchawi wako mimi Mimi hasidi yako mimi Mimi na ubaya wako mimi Kila kitu mimi Pole, pole sana eeh Pole, pole sana eeh Kuna nazi, kuna nazi Kuna nazi, haya kuna nazi Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe Kama hujui nenda muulize somo yako Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe Kama hujui kamuulize somo yako wee Mi mwenzangu anakuna nazi, haya kuna nazi Haya imba mwenzangu anakuna nazi, haya kuna nazi Nazi kweli jamani inampendwa wewe Ila kukuna eeh yahitaji ujuzi wee Na iwapo wataka kujaribu wewe Basi nenda uulize wenye ujuzi wee Angalia usilete upuzi wewe Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wee Mi mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi Haya sasa mimi na kuna nazi, haya kuna nazi Kukuna nazi kwahitaji ujuzi wewe Kama hujui nenda muulize somo yako wee Mi mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi Mi hodari kukuna ee kuna nazi, haya kuna nazi Haya imba mwenzangu ana-kuna nazi, haya kuna nazi Sitaki, sipendi, naogopa Anajijua yeye kwamba yeye si mzima Anataka kumpa mwenzake maradhi Anajijua yeye kwamba yeye si mzima Anataka kumpa mwenzake maradhi Kwa makusudi Sitaki, sipendi, naogopa, sitaki Anajijua yeye kwamba yeye si mzima Anataka kumpa mwenzake maradhi Anajijua yeye kwamba yeye si mzima Anataka kumpa mwenzake maradhi Kwa makusudi Sitaki, sipendi, naogopa, sitaki Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Maneno ya watu wanapenda uwongo (hicho kiranga) Ua fisi wapi? Kutwa kimbelembele (hicho kiranga) Watu washamjua pembeni wanamcheka oooh Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Ugomvi si wake kutwa kimbelembele (hicho kiranga) Kuchukia watoto wa wenzake bila sababu (hicho kiranga) Kuingililia maneno yasiyo mhusu (hicho kiranga) Wenzake washamjua pembeni wanamcheka Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Umelikoroga hilo, leo utalinywa hilo Chachizi ukimpa tatizi alitatue ni tatizi (haha)