Kitambo bado vita itaisha, kitambo, na dhoruba zitapoa Na tena nitalaza kichwa changu mbavuni mwake anayenipenda Nitaziona raha na amani, mbinguni hazitakuwapo dhambi Kitambo bado roho yaumizwa, kitambo katika usiku huku Machozi nina'toka mara nyingi sababu sijaona bado Yesu Lakini asubuhi ya milele huko mbinguni sitalia tena Kitambo bado ya kuchoka huku, kitambo, tena nitaona Yesu Na huru mbali na hatari zote nitastarehe mikononi mwake Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli Mateso yangu hayadhuru tena, nitasahau yote kwa Yesu Nikisumbuka mda duniani, mbinguni sitaona shida, kufa Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote