Nakiri nilikuumiza sana mama yangu Nyumbani kukugonganisha na machangu Pia kukugombanisha na ndugu zangu Ili mradi nifurahi ndani ya nafsi yangu Nakunywa ninalewa na rafiki zangu Nakuangushia kipigo na una mimba yangu Mpaka mimba ikachoroboka kwa ujinga wangu Leo nitaficha wapi mimi sura yangu? Mbele sioni kitu zaidi ya ukungu Na maadui wako wengi zaidi ya nywele zangu Nishike mkono mikosi inaniandama Na usipo nionea huruma haki ya nani nitazama Mwili hauna nguvu kama mwenye homa Nahisi niko kuzimu na shetani ananichoma Ongea chochote na nafsi yangu itapona Nakiri sitorudia tena mbele ya Maulana Najua unanisikiaaa Ila kunijibu ndo huwezi Eeeh Mungu baba saidiaaa Umlaze mahala pema mpenzi Na pia anisamehe maha, anisamehe Na pia anisamehe sana, anisamehe Nisamehe nitakufa, kwa mawazo ya msongo Wapambe walionipamba, wamenigeuzia mgongo Baada ya kuishiwa pesa, wanadai sina mpango Ni kweli sina dini, wala sina mchongo Siku hizi sinywi bia, ni viroba mixer gongo Nisikufiche, nimepoteza malengo Kwenye kupa kwa mizigo, kwenye lori mi ndio tingo Maisha yangu yanaelekea ukingo Na kama nitakufa leo, jua kuu uliacha pengo Nikiongea sana nikajitukana Maana nilifungwa macho na starehe za ujana Nikajiita pimpi kicheche bonge la bana Nikakupa mateso ya moyo, mwili kimwana Na kila nilipolewa ni kichapo cha kufana Nishike mkono japo nimelewa sana Sema neno moja liuponye mwili wenye laana Najua unanisikiaaa Ila kunijibu ndo huwezi Eeeh Mungu baba saidiaaa Umlaze mahala pema mpenzi Na pia anisamehe maha, anisamehe Na pia anisamehe sana, anisamehe Nakiri sina uti, ila sasa nakwangukia Unanijua vizuri, sina haja ya kuhadithia Ila sirudii makosa haki ya Mungu naapia Sauti za kuzimu ninazisikia Bila msamaha wako hakika nita disappear Mi kipofu niongoze, natanga sioni njia Nakiri mi ni bonge la fala tena mburula Nilikuona taka-taka nikazurura Nikapiga chaka kwa chaka na kina Shura Sasa cheki nilivyo, nimenyooka kama rula Natamani ardhi ipasuke nijifiche sura Ama kweli dunia imenielemea Mzigo ni mzito Golgotha naelekea Ndugu wa damu yangu, sioni walikoelekea Hakika ni wewe pekee unaweza kunitetea Nadhani sasa sina tena cha kuongea Najua unanisikiaaa Ila kunijibu ndo huwezi Eeeh Mungu baba saidiaaa Umlaze mahala pema mpenzi Na pia anisamehe maha, anisamehe Na pia anisamehe sana, anisamehe