Hili joto hasira (amba)
Upepo hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba
Foleni njia mzima (amba)
Na pesa hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba

Kila siku nimenuna kwanini tunagombana
Tena tunakosoana kama tumechanganyikiwa
Na sioni hata maana ya si kuzinguana
Yaani kila mtu anajua sana
Au yote sababu ya sababu ya

Hili joto hasira (amba)
Upepo hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba
Foleni njia mzima (amba)
Na pesa hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba

Mazao twalima wote, sahani wavuta kwako
Kama chakula tule wote, kwanini chote kije kwako
Kisu mpini umeshika wewe, ni tishio kunikata mimi mh
Au yote sababu ya sababu ya

Hili joto hasira (amba)
Upepo hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba
Foleni njia mzima (amba)
Na pesa hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba

Sahau sahau shida ooh ziliisha jana
Say goodbye joto, rest in peace shida
Knock, knock money

Profesa Jay
Wenyewe wanasema usawa unakaba
Na rafiki wa kweli ni mama na baba
Hawa wengine wala usiwaamini
Binadamu wa sasa wana roho saba
Watakuwa na wewe kwenye raha
Na hawatakuwa na wewe kwenye njaa
Bora nipige misele yangu peke yangu
Niruke peke yangu uwoga niliukataa
Nabadilika kama saa na siku hazigandi na sitakata tamaa
Wamejaa usaliti na chuki
Watu wa karibu wamegeuka mamluki
Boom! General nasonga
Iwe joto au baridi naamini tutashinda
Kama mbwai iwe mbwai barida
We make more money rest in peace shida
Ukinuna unataka tunune wote
Ukilia unataka tulie wote
Vita vyako tunapigana wote
Tukishinda tushinde au bora tufe wote
Kama kulima kote tumelima wote
Hata kupanda kote tumepanda wote
Kupalilia tumepalilia wote
Aah nashangaa sasa mbona hatuvuni wote

Hili joto hasira (amba)
Upepo hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba
Foleni njia mzima (amba)
Na pesa hakuna (amba)
Naruka mwenyewe yerela, yerela, amba
    Página 1 / 1

    Letras y título
    Acordes y artista

    restablecer los ajustes
    OK