Umepika chakula huli, huoni chapoa?
Umpweke, mwenye moyo wa duni, twakuita soledad
Kula dada kwani huyo haji, eti yuko na washikaji
Na akirudi matokeo yake ugomvi hauishi
Uko alipo mbali na upeo wa macho yako
Atafanya baya atakalo bila idhini yako
Unangoja na kusubiri, utasubiri sana
Hatokeo kwako machoni hutomuona mwenzio

Uko na rafiki zako, kwako nyumbani kitako
Mkipeana michapo, huku mkicheka na vicheko oh
Wawapa habari zako, jinsi bwana anavyokutenda
Hutojua moyo wake, kwani ni vigumu kufungua moyo

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo

Mmelala ni usiku sana, usiku wa manane
Akili yake kumbe yamuwaza akiwa na mwingine
Milio ya simu na ujumbe mfupi vinazidi kwa sana
Ukimuuliza bwana kulikoni utaambiwa ni story
Nao moyo wako punde, unaanza kwenda mbio
Mara usiku akuage kuwa anakwenda kutukio
Muulize ni wapi pande, hatokujibu mwenzio
Mara na siku zingine simu yake iko bize nusu saa

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo

Angejali moyo wako, asingekuumiza huyo
Angeacha atendayo ili wewe upate faraja ah
Lakini umuulizapo, juu yeye hukujia
Hathamini chozi lako, na wala halijali hilo lako pendo

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo
    Página 1 / 1

    Letras y título
    Acordes y artista

    restablecer los ajustes
    OK