Spice music Maisha yangu si ya ki papa Ni vitembele ya nyanya chungu Dagaa kurusungu, hummh Niko chakavu na nimechakaa Yaani naishi ki mungu mungu Mtetezi wa bunjuu Mjukuu wa binti simba Okoa mangala Wa mwisho kitinda mimba Mwenye elimu uchwara Maisha yalivyo nifilimba, akanijalia jallah Nikaanza kuimba, uniondoke ufukara Ila bado Kipato changu cha chini nacho kina utata Hata visenti hamsini kuvipata mashaka Nalia na umasikini mungu ashushe baraka Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa Tukaze roho, tukaze roho tusichoke Tukaze roho, mungu wa kwetu sote Tukaze roho, eeh tusichoke Tukaze roho, mungu wa kwetu sote Mmh Japo, maisha yenye ya manati Hatupati kila tukilenga Kukicha misumari ya bati Kuku kapenya kwa tenga Kula yetu tu ni wasiwasi Tutapata wapi ya kujenga Wa kupiga picha masaai Kulala mbagala kwa chemba Tunaunga unga mwana (haya ndo mambo yetu) Hayana tofauti na jana (ndo maisha yetu) Wazazi kulala na mwana (heey) Chumba kimoja mandoo, masufuria (wenyewe tushazoea) Kipato changu cha chini, nacho kina utata Ata visenti hamsini kuvipata mashaka Nalia na umasikini mungu ashushe baraka Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa Tukaze roho, tukaze roho tusichoke Tukaze roho, mungu wa kwetu sote Tukaze roho, eeh tusichoke Tukaze roho, mungu wa kwetu sote (Ayolizer) Wanangu wa bodaboda, tukaze roho Kina mama vikoba, tukaze roho Ah rumbesi wabeba virogha, tukaze roho Vijana wezangu, tukaze roho Tutapata tu