Mama mwenye nyumba Mwenye nyumba, mama mwenye nyumba utaniua wee (Next Level Music) Nusder! Mi najiuliza maswali, nihame niende mbali Kwa visa unavyonifanyia mama (Mama) Mi namlaumu dalali, ndo kaniletea shali Mitego imenizidia jama, (Jama eeh) Ah ah, kiti kipo hakai Akifua akipika nainama Mama kiboko, mama kiboko Jana kaniletea chai Leo kaleta ubwabwa na nyama Na kangamoko, na kangamoko eeh Anavyonipa mashawishi mwishowe nashindwa jizuia Yatanifika mazishi mumewe akinifumania Kasema hamfikishi mzee Ana tumbo la bia Mama anataka mwichi yaani kisu kikachane pazia Aah niue nisiue? Ua! Mwanamke wa mtu sumu Kuna jela na gesti Ndani nyumbani nina majukumu Aah niue nisiue? Ua! Wasije kunivukia dumu Wazee wa vilainishi Wakapita Mombasa na Kisumu Mama mwenye nyumba Mwenye nyumba, mama mwenye nyumba utaniua wee Mama mwenye nyumba Mwenye nyumba, mama mwenye nyumba utaniua wee Nikimpa kodi anakataa, anairudisha eh Bill ya maji, bill ya umeme anazirudisha eh Nikimamkia anakataa, anajinunisha eh Kweli ngo'mbe hazeeki maini anajibebisha eh Usiku anagonga milango anakuja tuputupu Ananizuga samaki chambo, tucheki movie za rufufu Hajui nimetoka jando, ananifosi mabusu Nisije nikampa tango nikaishia kisutu Nikileta vimada visa, majanga shetani kapandishwa Oh mama mama yeah, mama yee Hakaukagi kujipitisha, wivu ndo unamkasirisha Oh mama mama yeah, mama yee Aah niue nisiue? Ua! Mwanamke wa mtu sumu Kuna jela na gesti Ndani nyumbani nina majukumu Aah niue nisiue? Ua! Wasije kunivukia dumu Wazee wa vilainishi Wakapita Mombasa na Kisumu Mama mwenye nyumba Mwenye nyumba, mama mwenye nyumba utaniua wee Mama mwenye nyumba Mwenye nyumba, mama mwenye nyumba utaniua wee