N-Next Level Music Hmm mmh, ohhh (Ayolizer) Mmmh, siri ya mwezi Siri ya nyota, siri ya angani Siri ya njozi, usingizi Siri ya kitandani Ila siri ya penzi, siri ya moyo Siri ya nani? Siri ya chozi, ni maumivu, ndani kwa ndani Mapenzi niliyaanzisha yakanifurahisha Yakanibadilisha jamani Na sio tu kumridhisha Nikamthaminisha, nikamtambulisha nyumbani Hasa leo yamekwisha yananidhalilisha Yananiaibisha hadharani Ila yote ni maisha, japo nahuzunika Wakuninyamazisha ni nani? Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini Kasuku ndege wangu, leo umekuwa bundi Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi Ile siku unafungasha mabegi Ulidondosha picha yako njonjo Ndo ninayojilazia kwa bedi Haki ya Mungu umenipiga zongo Naomba msalimie shemeji Haki ya nani amepata chombo Na kama ukiskia nimededi Jua ni mawazo msongo Nenda, salama nenda Nenda, salama nenda Nenda, salama nenda Nenda, salama nenda Nikiwa na marafiki, kwenye sura naogopa Ila moyo unasota Nikiwa peke yangu siwezi Chozi linanidondoka Nahisi kama naota Hivi kweli umeondoka? Yanautesa moyo mapenzi Mpaka kupenda naogopa Umesema, hutaki tena kuiona sura yangu Kwenye simu umefuta namba zangu Ila jibu lipo kwa Mola wangu Mi nasubiri Kila baya, unasema ukitaja jina langu Umesahau yote mazuri yangu Basi nilindie madhaifu yangu Unisitiri, maana Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini Kasuku ndege wangu, leo umekuwa bundi Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi Ile siku unafungasha mabegi Ulidondosha picha yako njonjo Ndo ninayojilazia kwa bedi Haki ya Mungu umenipiga zongo Naomba msalimie shemeji Haki ya nani amepata chombo Na kama ukiskia nimededi Jua ni mawazo msongo Nenda, (hey) salama nenda (Nenda salama, aaah) Nenda, salama nenda (oooh, oooh) Nenda, (ouuuh, oooh) salama nenda (Nenda salama, aaah) Nenda, salama nenda (Nenda salama, mmh oooh) Mwenzako naogopa, -ogopa eehh, iyeaaaaah Mmh oooh Kila baya, unasema ukitaja jina langu Umesahau yote mazuri yangu Basi nilindie madhaifu yangu Unisitiri (Ka mix Lizer)