Nina imani nitafika Jibu ni kufika Japo uwoga na wasi wasi Nitafika niendapo Jibu kwa moyo mwangu, nitafika eeeh Natamani kuenda kule nionapo Nina shauku ya kutekeleza Maono yangu eeh Lakini vikwazo ni vingi sana Lakini majaribu ni mengi sana Oooh wa kunivunja moyo Ni wengi sana njiani Pharao na jeshi lake hawataki kuniacha Jibu kwa moyo wao, nitafika Japo milima na mabonde Nitafika nitafika niendapo ooh Nahitaji nehema yako Jehovah Nifike niendapo ooh Nahitaji msaada wako baba Nifike niendapo ooh Naomba nishike mkono Nifike niendapo Jibu kwa moyo wangu Nikufika Bado nina pumzi, tumaini langu lipo (nitafika tu) Sikupata leo, kesho inakuja oooh (nitafika tu) Baada ya kesho, mwezi ujao unakuja (nitafika tu) Najipa moyo mwaka kesho nitafaulu eeh (nitafika tu) Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe (utafika tu) Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu) Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu) Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu) Nikufika nikufika wee (utafika tu) Nikufika nikufika wee (utafika tu) Ata usiku uwe mrefu kutakucha Ata giza iwe kubwa nuru itatokea Jibu ya maisha yako ipo leo Ata safari iwe na vikwazo utafika Hata jaribu liwe nzito utavuka Jibu ya maisha yako ipo leo Unamkumbuka Sara alipata mtoto uzeeni Unamkumbuka Hannah mpaka alichekwa oooh Kumbe tumboni mwake amembeba Samweli Nehema ya Mungu bado iko nawe Yamkini huduma yako imebeba vitu vingi Hata giza liwe kubwa nuru nayo ipo Nehema ya Mungu bado iko nawe Hata maji yawe marefu basi kuna ukingo wake Nehema ya Mungu bado iko nawe Huruma ya Mungu bado inakutafuta aah Nimejitahidi sana bila mafanikio (nitafika tu) Haijalishi shida, vikwazo safarini wee (nitafika tu) Sijali wangapi wananikatisha tamaa (nitafika tu) Wala sitajali mazingira ninayoyapitia (nitafika tu) Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe (utafika tu) Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu) Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu) Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu) Nikufika nikufika wee (utafika tu) Nikufika nikufika wee (utafika tu)