Mwenzako nishaanza mwanzo
Sikufichi hope hata kwa macho
Simu ishaisha bundle
Yanini vijembe mipasho

Ata mwenzako sifikirii bado
Matapishi sirudii
Naona unazuga zuga bado
Kumi na nane siingii

Hasira hasara
Kupenda sana ukaninyanyapaa
Nami nikaona haina maana
Nikajitoa unataka rudiana
Mbona kwangu mi?

Haina haja, haina haja
Aah nishamaliza, haina haja
Mbona kwangu basi, haina haja

Nilikupa unachohitaji
Mwenyewe nikajinyima
Ukanishusha na hadhi
Ukanikosea heshima

Labda nikuweke wazi
Muda wa kupoteza sina
Ushamwaga maji
Yamenisomba na shina, ayee

Siwezi ng'ang'ania bango
Kuishi na wewe ka mapambo
Mimi natia nia unatania eiye yeah, yeah

Hasira hasara
Kupenda sana ukaninyanyapaa
Nami nikaona haina maana
Nikajitoa unataka rudiana
Mbona kwangu mi?

Haina haja, haina haja
Aah nishamaliza, haina haja
Mbona kwangu basi, haina haja
    Página 1 / 1

    Letras y título
    Acordes y artista

    restablecer los ajustes
    OK