Umeniburuza ka kitoroli Kutwa kunipeleka puta Ile sandaka lawe Ukaniona mpori pori Kukupenda ukavimba kichwa Leo bora ninawe Sikudhani siku moja Kama nitakuja toa machozi Kwa ajili yako na nilalame iyeee Kukuganda ka ruba Kuonyesha upendo hukujali Kabisa maa ee, ooh maa eeh Natembelea magongo (aah) Mzima bado nachechema (aah) Ila kwa hali sio shwari Nisije nikatoka chongo Kwa mapenzi kung'ang'ana Nikadhoofu hali Nalia mwenyewe, mwenyewe Japo nina ugonjwa moyoni sijui lini nitapona Nalia mwenyewe Mgonjwa nakatisha dozi bora nitoweke duniani Nalia mwenyewe, mwenyewe Mgema kasifiwa pombe kaitia maji nanyotokwa Nalia mwenyewe, nitazoea hali yangu Don't cry baby, we unadhani itakuaje Ukiondoka ukasepa na moyo wangu mfa maji Don't cry baby, we unadhani itakuaje Ukiondoka ukasepa na moyo wangu mfa maji Si unataka kunitosa Na unajua mapenzi hayana kocha (kweli nimekubali) Najua umechoka For the first time natambua makosa (kweli nimekubali) Mwisho wa wiki hazikuniisha safari Vishawishi kasababisha dosari Najikuta nagonganisha magari Ooh mama ma Hapo sasa umenishika sharubu Tungi tungi nyumbani unafanya kusudi kunisulubu Tumpe faida nani? Mdomo juu juu unataka niwe bubu Siwezi kukuchapa makofi utakuwa sugu Kwanza mapenzi matamu kati ni msala Unapopungua upendo na kugeuka biashara Kosa pesa ulale kwenye kochi Kodoa macho tochi Nalia mwenyewe, mwenyewe Japo nina ugonjwa moyoni sijui lini nitapona Nalia mwenyewe Mgonjwa nakatisha dozi bora nitoweke duniani Nalia mwenyewe, mwenyewe Mgema kasifiwa pombe kaitia maji nanyotokwa Nalia mwenyewe, nitazoea hali yangu