Nderemoo, na vifijo si mayowe Te amo, furaha yangu kupendwa na wewe Maneno wasemayo na yapuza ujue Sikurushi roho nikuache uumie Na sina sifa ya kuku Kila da ni nipakue mie Wala lopo ya kasubu Ya watu niyahadithie Upole wangu tausi Vigengeni hunikuti Na sina huba la nuksi Nakshi zangu ni marashi Sawa Kusemwa nishazoea Haya Mwenzako nishazoea Sawa Kusemwa nishazoea Haya Mwenzako nishazoea Mi sitovaa vimini vya mpasuo kwetu mwiko Natinga baibui mwilini na videra vya baikoko Tena najitia uturi viyasmini vya mtoko Nikupeleke nyumbani Kisiwa cha karafuu Tukale madoriani Shoki shoki za udambu Jioni twende forodhani Tukale upepo mwanana Chaza mchukue mwambani Na iwe zawadi ya mama Upole wangu tausi Vigengeni hunikuti Na sina huba la nuksi Nakshi zangu ni marashi Sawa Kusemwa nishazoea (aah ahh ah) Haya Mwenzako nishazoea (nishazoea mie) Sawa Kusemwa nishazoea (ooh ooh oh oh) Haya Mwenzako nishazoea (nishazoea miee eeh)