Sasa kila kitu doro Tumevumilia kwa maisha tumetusua Tulivyokula kiporo Nilifikiria tunda watalichukua Hakuna tena sorrow Ni muda wa kujivunia na kutulia Shopping twende Comoro Na unachofikiria nitakununulia Maisha yetu tamu yaani tende Sina sababu yaani bora nikupende Wewe ni kichwa mimi ni pembe Kama penzi nitakupa tamu usiende Ya habibi Ni wewe umenivumilia Sina budi Kukuwa nawe beiby Ulinishika nikashikilia, tukapenda Hawajui tulipoanzia, wanasengenya Mahaba we wanijulia, unazo tekenya Unapotaka tutaishia, daima kwenda Ooh beiby beiby na wala usione ghari Kwa hiyo maisha tunayokaa Ooh beiby beiby ukitaka pia magari Ukitaka juu tunapaa Kila kitu sawa (sawa) Usijali mama kila siku uko na mimi Yaani sawa (sawa) Unachokipenda utakipata hapa mjini Nasema sawa (sawa) Tumetoka mbali sitakuendea pembeni Nasema sawa (sawa) Yaani sawa (sawa) Mi napenda unavyonukia Urembo wako wee wavutia Macho yako ukiniangalia Moyo wangu unatulia Kisura mi nagharamika mwenyewe Kwanini nisiwe na wewe Ka ni wakufura, tumeteseka wenyewe Waache wasituelewe Inshallah Mola tumuombe Akuondolee Maisha mema tuendelee Nyuma tusiregee Ya habibi Ni wewe umenivumilia Sina budi Kukuwa nawe beiby Ulinishika nikashikilia, tukapenda Hawajui tulipoanzia, wanasengenya Ni mahaba we wanijulia, unazo tekenya Unapotaka tutaishia, daima kwenda Dunia ilinifunza Ila wewe ukatulia Sasa nakutunza Na maisha twaurahia Kila kitu sawa (sawa) Usijali mama kila siku uko na mimi Yaani sawa (sawa) Unachokipenda utakipata hapa mjini Nasema sawa (sawa) Tumetoka mbali sitakuendea pembeni Nasema sawa (sawa) Yaani sawa (sawa)