Alilililii (Ayo lazer!) Furaha isio kifani, kumpata mwandani Hakika wamependeza Ngoma lipo uwanjani, kaibiwa nani Sa unaachaje kucheza Hama kweli harusi imefana tena ya kihistoria Pande zote, baba na mama, naona wanashangilia Ila sitaki kua mnafki, Jumba bovu kuniangukia Nina langu la moyoni, ningependa kuwaambia Bi harusi, mashoga wakupupia Hao niwakuwaangalia Wako wale wahali gani, wanakuja kuchungulia Uwaombe samahani, uwakomeshe wambea Eti, wifi umepika nini, na mimi utanigaia Waambie, wamepika p dagaa, zenye pilipili nyingi Zakutisha we na mumeo, wao watakimbia Aii shemeji Ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani Na hii ndio meseji Sema na mumeo usifuate ya jirani Kwa furaha niliyo nayo Niacheni nimwage radhi (alilililii) Mi nataka nimwage radhi (ai yoi yooo) Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi (alilililii) Ng'ombe anapoita ndama, tunasema kua analia Kupigwa na kulalama, hatujawahi kusikia Hakika mmependeza Ninavyomfahamu biharusi, sipati kusimulia Nimetoka Ruvuma, Mchomori, namtumbo Lindi, mtwara mpaka chitohori nimezisikia Sifa za binti huyu, Mola amemjalia Binti hapendi majungu, hakika ninawaambia Ukimuazia viatu na gauni, anakuachia Bwana harusi tunakupa mke, ukaishi nae vyema nyumbani Huna kitu usimfiche mwambie, taabani Ikiwezekana mkakope, mkono uende kinywani Usimpige mateke, kisingizio kitu fulani Ooh umefanya nini jana, hakuliki leo ndani Mtoto bado mteke, usimkomaze Kwa ngumi Ukimshindwa mrudishe, kwao hajaua huyu Mumeo akienda kazini, akirudi salimia Wala usikae chini, chakula kumsukumia Bali mkaribishe ndani, hali kumjulia Muulize za kazini, kwa tabasamu muruua Kisha msindikize bafuni, hata kama anapajua Halafu wewe tafuta kiti, jikoni kimbilia Chukua simu yako message, ukimtumia Mwambie hasilani bila wewe, chakula hakitaingia Eh! Aii shemeji Ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani Kwa furaha niliyo nayo Niacheni nimwage radhi (alilililii) Mi nataka nimwage radhi Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi (alilililii) Nawaomba niishie hapa tarishi huwa hafungwi Naomba nichape lapa, yaliobaki ni ya makungwi Niliowakera samahani kusema ni jukumu langu Nawaomba muishi kwa amani hio ndio furaha yangu Mmh ndio ni kama safari tuombeane dua Atuepushe na shari saa chini ya jua Aah somo yake mwari, ainuke Mama yake mwari, ainuke Baba yake mwari, aunike Aje kati tuicheze ngoma Aah kaka yake mwari, ainuke Dada yake mwari, ainuke Shangazi yake mwari, ainuke Aje kati tulicheze ngoma Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi Niacheni nimwage radhi Mi nataka nimwage radhi