This is another one Wengi wanakuombea utupu so piga kazi makini Maana mtegemea cha ndugu heee utakufa maskini Ndo maisha ya mjini changamoto mimi na wewe Japo tulianza kuwa moto kabla ya moto wenyewe Ndoto yangu ya milele sio tu kuimba na kuparty Maaana mziki ni zaidi ya maisha kuvimba na magari Bro, hili dili hatari fans kuja show shida Wanasubiri ufe uweke rekodi ya kujarida Sa mwelewe wazee mnapunga, pendeza wezeenu na nyumba Ata sauti ina paa mzee ila huwezi kuwezeka nyumba Huwezi kung'oa mchumba kama hauna doh mingi Utaishia kujidunga bro maana stress ni mingi Na mawazo kishimule, kichwani hauna shule Dem wako anajiuza half na bei ni kama bure Ndoto ukiwa nayo shule, hello ndugu na yaya tule Walo kufa wote ni wajanja ndo maana wamewahi kule Si since day one tupu zetu Na wanaume waloshindwa kumpa mimba Wema Sepetu Bigiri yechu yechu Shida, mwisho wa siku tunalia U superstar mwiba, mzigo wa mwiba tunaubeba tunaumia Mwanzo niliwaambia, ila kupitia haya mtakiri Kujiongeza kwenye hakuna, tumizi mbaya la akili Je hukubali kuuchuna huo upande wa pili Wasikusemeshe ka mtu hajapiga mswaki wiki mbili Namkiri ipo wazi hatuhifadhi makua Kina sisi hatuna target tutoe wapi? Nafuu Nipeni pasi ninyooshe miguu Bwana mwane'nu nimejua kuwa dwanzi ndo ako ngazi za juu Mara hiphop haiuzi asa hiphop ya juzi kina Young Killer ndo mnaongoza kutoleta michuzi Mara hiphop ime loosi ati hatuna ufumbuzi Akina sisi hatuna Swagga sijui mpaka tufanyeje music Huo ni uwongo na mnajua Hakuna ashindwalo Mungu akitaka inakuwa Dunia changamoto na maisha ni hatua Alopitia tangu mtoto mpaka anakua Mpaka anajua raha mechi kibao Akipata kifua chumvi limao Sa hivi Simba na anambao ndo hashindani Ila Barcelona Arsenali ndo level za jangwani (Young Africa) Mbona uwe fahari kwa wenzio michezo ya namna hiyo Hatuikubali ni ya kidem Ni sawa na kusema we ni mkali wakati sio Na redio zinakupea promo hatari unauwa game Asa kipi bora uwe na furaha na umekwazika Ama uone kinyaa ati uwanja umetapika Maana ina fahamika Mziki nao mziki na mchwano ni mkali kati ya biashara na hailipi Biashara imeshindwa la lahaula inang'ara Wa mabingwa wanalindwa kama Paula Wakajala Alafu wanatuweka roho juu kwa mikwala Wakati tunajua hawakosi show tu wanakosa hadi pahali pa kulala Wasanii uchwara, wasanii hawajala Wasanii wana njaa wameshaweka duara Wasanii mafukara, Bongo wasanii mikwara Hao wasanii wametia kila kampuni hasara Bongo noma regeza mjini Babu unachekwa Uliza Roma kwani alifanyiwa nini baada ya kutekwa (Well, well, well) hio ni siri ya kambi Na kuto waheshimu wakubwa hio ni akili ya bangi Ila akili ya Mange ni kufunguwa duka Ila asili ya rangi nyeupe ni kuchafuka Akili ya msomi ni kujijengea future Ila akili ya mjinga ni kutaka vyote kwa pupa Kwa hiyo anakosa vyote Na siku ndo inavyokuwa show zangu natisha Ila Izraeli ndo anaye ua Mungu ndiye anaye jua, upi mwisho wa mimi So ananipenda ananilinda yuko pamoja na mimi Alafu mi najituma bwana, nasema mi najituma Nipate kusimulia nikipata jukuu zangu Mi ni msukuma bwana, nasema mi ni msukuma Ndo kitu me najivunia usukuma fahari yangu Japo nasikia, wanasema natoa ngoma hazibambi Cjai diss iwa na Mange Nakula sana stori lakini sio eti kitambi Sina shawty ati nitafte kadem ati nikala Nandy (alalalala) Acheni shetani apite hoja zingine za kike Mi mmoja kati wanofanya hiphop isikilizike Kwa hiyo staki tungombane ya nini tuchoshane Usibebe tango lote baby kaa vipi tukatiane If you love me, love me and show me your feelings And if you don't talk, you will die alone Cz always machungu yanabaki kwa watawaliwa And we need love revolution man Hey greatest It's time to wake up and watch Young Killer Msodokiii!