Tarara tarara tara Ndoto niote eti mimi napepea Maombi mniombe muziki nizidi bombea Hutoweza kurekodi kama huna cha kuwapea Niuze sura nione kama watainunua Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume Si rahisi kwenye Twitter waseme kanadia katambe Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi Si rahisi, si rahisii Nilifunga safari eti naanza kuimba Nikajiona wa kusifiwa kama papa wemba Ngoma zangu zivuke border mpaka kule pemba Ujumbe nao usikike kote mpaka na wakamba Ilinivunja moyo waliponifukuza studio nitoke Wakanidharau familia ndugu wa toka nitoke Promoter bandia kunipa show kisha jioni apotee Producer chocha niimbe lingala, nazali nayo mboote Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume Si rahisi kwenye Twitter waseme kanadia katambe Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi Si rahisi si rahisii Kwenye industry wanatuchesa, controversy zilete pesa Eti kanadia naye yule, mara nimetemwa vilevile Wengine wavume bila talanta Kwenye picha tako wamekamatwa Jina tupu walishapata, je huu ni ungwana Eti muziki kizungumkuti Ikinishinda niipige buti Ama nianze kucheza isukuti wee Tena yao beef sijazoeaga Mi ni mpole wananianzaga Eti sanaa nianze kuaga Haya maneno zilizaga we Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume Si rahisi kwenye Twitter waseme kanadia katambe Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi Si rahisi, si rahisii Ata nikifa leo niwe wa kusifiwa Niliishi kutamani niwe kama Miriam Makebaaa Si rahisi nisikike, si rahisi nivume Si rahisi nikubalike Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume Si rahisi kwenye Twitter waseme kanadia katambe Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi Si rahisi, si rahisii Cherie, cherie, si rahisi eeh Si rahisi eh