(Eyoo Trone) Heshima na upole wako Ndivo vikanivuta kwako oh oh Tabia na mwenendo wako oh Vikanifanya nikupende eh eh Kumbe mapenzi ni nyakati yanachanganya Yakipoteza ramani wewe Kitabu cha upendo wa dhati umechanachana Haupo kama zamani wewe Ngoma ikivuma mwisho wake hupasuka Yote ya nini tuje kushikiana chupa Wewe ukipanda kila muda mi nashuka Oh ooh oh, oh oh oh Message za watu wako na simu zako Naona ila namezea tu Najua machafu yako mabaya yako Yanachoma mi napotea tu Kugombana mi siwezi Nikwambie yote sababu ya mapenzi Tena narudisha jezi nitulie Ligi ya mapenzi siwezi Kwako wewe, bora peke yangu Nibaki pekе yangu Bora peke yangu Niishi maisha yangu Bora pekе yangu Nibaki peke yangu Bora peke yangu Niishi maisha yangu Uliweka pamba masikioni Husikii huoni ninavyoumia moyoni Purukushani asubuhi jioni Matusi mdomoni hata aibu huoni Ukadanganya unaenda sokoni Kumbe yuko mgongoni kitandani ukingoni Una wapenzi wengine kinondoni Hadi Kigamboni na Kariakor shimoni Ah wee, kumbe ni mnyama uloficha makucha Hata sura yako inakusuta Nyama ndani ngano nnje kama sambusa Barafu wa moyo umeyeyuka (Oh wo wo wo wo, oh wo wo wo wo) Hukunipenda, pengine nilikulazimisha Sawa nakwenda, japo sina wa kuninyamazisha Huna makosa najilaumu nini? Nilikupenda kwa nini? Ona kugombana mi siwezi Nikwambie eti sababu ya mapenzi Tena narudisha jezi nitulie Ligi ya mapenzi siwezi Kwako wewe, bora peke yangu Nibaki peke yangu Bora peke yangu Niishi maisha yangu Bora peke yangu Nibaki peke yangu Bora peke yangu Niishi maisha yangu (Nusder)