Corona, corona, corona Corona, corona, corona Wote tumuombe Mungu kwa hili janga Ikibidi lipite Tujihadhari na tujikinge Ili lisitufike Habari kote duniani zimesambaa Ugonjwa unaua na hauna tiba Na wengine wetu masikini hatujiwezi Mwenyezi Mungu kawe tiba Watoto wetu mashule, aah Mama zetu tu sokoni Kwenye vyombo vya usafiri makazini Tujilinde Osha mikono (aah) Epuka mikusanyiko sio ya lazima (aah) Na uonapo dalili Mapema wahi hospitali Corona, corona, corona Corona, corona, corona Corona, corona, corona Corona, corona, corona 'Hatua zimeshaanza kuchukuliwa Ameshatoa tahadhari mbalimbali Ambazo tunatakiwa kuzichukua Napenda nirudie ndugu zangu Watanzania Kwamba ni vizuri sana tukaendelea kuchukua tahadhari, kwa nguvu zote Ugonjwa huu unaua, na unaua kwa haraka sana Niwaombe ndugu zangu Watanzania Tusipuuze ungonjwa huu Tusipuuze hata kidogo Ni lazima tuanze kuchukua hatua Za kujikinga kwa tatizo hili Corona, corona, corona Corona, corona, corona Corona, corona, corona Corona, corona, corona