(Tongwe Records) Ooii naona mtandao unakatika Upo kimya sana mkato au kunde imevunjika Na mtanyooka roundi hii Na hivi huwezi bila mimi? Najikuta Jay Z oya unarudi lini? Kaka huku wamefunga mipaka Ila tiketi nilikata nirudi kabla ya pasaka Rudi ugeuze kisu sio Mwana wa kulitafuta mwana wa kulipata Round hii sio nunio, daraja la mpasu Kumekucha hivi saa ngapi huko nipe takwimu Nimeamka nishaweka bundle namngoja Umi mwalimu Anapambana yule dada Tanga nimewavulia kofia wametoa sanitizer za iliki Yaani ukipaka unanukia Hehehe Corona nishai yaani Bongo kila mtu daktari Masai kachemsha maji ya mpapai kanywa na sukari Guza hadi maski wanafua sijui ni nani kawafundisha Huku kuna dada kajifukiza mashetani kayapandisha Tueke siasa kando unajua uchumi unashuka Sio Bongo tu hadi ng'ambo watu wamefunga maduka Hapa nawaza pesa ya bango benki walokopa wanajuta Tukisema tukae ndani na hii njaa si tutakufa Hali inatisha na umasikini, tunaoumia ni sisi Yaani bora ufe kwa Ukimwi angalau utaandika urithi Kwa iyo hamna bata, sio kidimbwi sio tipsi Kaka madanga yamekata so hazitimbi hizo piece Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega nani kama wewe Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega nani kama wewe Hivi unakaa jimbo gani au Marekani Unajikinga vipi maana vifo vingi hadi siamini (Mmmh) Au umesharudi ipo zako Horohoro nini We bwana hebu niache mi nimeze chloroquine Umenikumbusha kweli Chloroquine ni dawa? Bado inafanyiwa uchunguzi ila haijadhibitishwa Ingawa ukinywa haitohatarisha ndio maana bado wanaigawa Mi ninakunywa maana nilishika uso kabla ya kunawa Eti unaweza ukawa nayo na usionyeshe dalili? Ewaah! Uko sahihi, na kingine kuhusu hili ni kwamba Mgonjwa wa Corona unaweza usimtambue kwa macho So mtu yeyote unayemuona mpe mita mbili toka kwako Na hiko kiVansileka ndo kinini baba wawili? Ni ventilator, ni mashine ka mapafu ya nje ya mwili Mmmh sijaelewa hebu nieleweshe kuhusu hili Naskia vinauzwa ghali basi viwe vingi Muhimbili Okay, kirusi cha Corona kinashambulia mapafu Ndipo zinaanza homa, kifua alafu Unashindwa kupumua na mwili unahitaji tafu Ventilator huingiza hewa na kuitoa iliyo chafu Tuepuke mikusanyiko ikibidi tukae ndani Tumeambiwa tujifukize hivi ni dawa unadhani? Ngoja kwanza, hivi fumigation (Mmmmh mmh) Baba ile inaua mende eti (Hahaha wacha utani) Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega nani kama wewe Bwana wa mabwana Mungu wa miungu Alpha na Omega nani kama wewe Maisha ya upweke yanasumbua ila siku zinapita Yule mkewe itunze pete Mtayamaliza na uhakika kaka Ila hatua dua haina haja ya kusikitika Ila navyokujua hujazini miezi sita? Kiukweli mi mwaminifu ingawa jogoo anawika Mama Ivan mbabaifu haku-cheat una uhakika? Kuna mchezaji wa Yanga namwona anapita pita Nitamkata kata mapanga yaani namuua na namzika Oyaah wape nyumbani basi pesa ya matumizi Kaka nitoe wapi na show hakuna siku hizi? Hali imekuwa ngumu hakuna pesa kila kona Kila mtu unayemdai naye anasingizia Corona Mbona sasa wanafunga shule na vyuo alafu bar hawafungi Mzazi atamlindaja mtoto na akirudi yuko tungu? Polisi India wanapiga watu wakisongamana Wao barakoa hawana, jua defender wamebanana Sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike Ila wauguzi wanajitoa sana, dah Mungu awalipe Wapinzani mnatangaza vifo walopona hamwatangazi Ah-ah wanasema wangeweka takwimu za wazi ingekuwa kizazi Kwa hivyo lockdown hakuna alafu umeona text niliyotuma? Ipi kwenye group mbona inbox hakuna? Ah naskia (Nini?) koyuzeka mbochi Maana uliko uliko usiongee sana inatosha Hadi papai lina Corona dah (Kaka tuchati) Mmmh ina mbuzi vipi? (Eeh eh kaka tuchati) Mwili umekufa ngazi (Kaka tuchati) Poa mwanangu tuendelee kujifukiza (Tongwe Records, Bin Laden)