Alikuja kama masii tukamchangia sadaka Tukamwona nabii aliyeshushwa siku ya pasaka Tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe Eeh-eh na bado wakamlaza nabii kifo cha mende Hivi unamkumbuka babu? Babu wa Loliondo Ah-ah yule mfugaji mwenye bleach la kikogo Watu wamekufa, watu wamefungwa, watu wamepoteza biashara Sasa umekaribia uchaguzi amerudi chama tawala Vipi dada yetu wa Igunga, mmh simwoni udangani Ah mbona ashapata mchumba sio viben 10 wa zamani Yule fundi gereji chawa, si kamateka bibiye Na wamefungua mgahawa, yaani wote mama ntilie Na kuna dem aliyeachiwa mtoto akaolewa na mtoto Akaachana na mtoto akabaki anamlea mtoto Hizi ndoa za mjini bwana, zinasikitisha Eeh maana hufungiwa chumbani na huvunjikia Insta So soka la Bongo linakwama wapi? TFF maanake nini Tanzania Football Failure, ndo nacho jua mimi Unamfukuzaje Amunike ili udhaifu wenu umvuge Wakati mlimpeleka mlevi ye akacheze namba ya Mkude? Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero Ukuta tunavunja kwa tindo Wameshapigwa guu wako telo Na kiki za kikolo Majita tushapiga kishindo Hili ni fagio la chuma Linang'oa visiki Safisha vichaka kwa moto Simba kageuka duma Jangwa halipitiki Ukitufuata umetoa boko Marehemu walimsema mnyonyaji, kwani mziki una maziwa? Sasa Mungu kamhitaji na bado hajafanikiwa Hivi unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo? Acha maisha yaendelee, jasiri ameumaliza mwendo Aliyeokota almasi mchangani alikuwa Miss Tanzania Na aliyekuja inunua dukani ni Mganda aliyekuwa na nia Ya dhati la pakato akatokea mara mia Akawatumia ila mwamba ni mnyanyasaji wa kijinsia Sa skiza man hii, vipi shem mama Ivan? Ah tupo tupo tu ila hatupo ka zamani Nawe vipi kwani, mbona wife simuoni nyumbani Hey chill man, sina majibu deal done Bungeni daily majanga, viongozi wameishiwa mada Hivi mbunge wako wa Tanga hoja zake unaziskiaga? Sa nitazisikiaje? Na Ana spika mbovu za wana kijiji Ila fundi wao anakuja soon kutoka Ubelgiji Nabii Tito na Dr Shika, tayari wamesahauliwa Mwenzao Mariamu, biriani anapika anapakuliwa Bongo bwana, ndo nchi inayosupport sana ujinga Utashangaa Amber Rutty kala shavu ubalozi wa kinga Yaliyosemwa yamesemwa Kazi kwenye mmezoea kutema Wakitaka tuyajenge tena Waambie muda sio rafiki mwema (Yeiye iyee, aah aah iyee) Kusema kweli hatuchoki Na kwenda jela hatuogopi Tutabanana ata kama hapatoshi Hatupindishi ata kwa dumba Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero Ukuta tunavunja kwa tindo Wameshapigwa guu wako telo Na kiki za kikolo Majita tushapiga kishindo Hili ni fagio la chuma Linang'oa visiki Safisha vichaka kwa moto Simba kageuka duma Jangwa halipitiki Ukitufuata we toa boko