(Fraga got the recipe) Waliniita kimbaumbau, kiguu na njia Ila nikadharau, nikapuuzia Leo kwao kafa nyau, yanawanukia Kwetu twafinya pilau, yametimia Ooh wanjara, walete bunyero ooh Mi nataka kulimwaga razi (na makagheroo) Waite na mapaparazi (wapate kero) Wale wenye magho ya nazi (bando la jero) Wapate vya kuperuzzi Habari ziende kwa ma ex Penzi waliodhulumu Tena nimepata tetesi Mmoja ataka kunywa sumu Kisaa jamani kisaa Nikauliza kisaa, kisa leo naolewa Naolewa, naolewa mie (ooh sheba) Naolewa, naolewa mie Nilikosaga na dira kwa maneno ya waja Ooh subira aah, mbele inafaraja Asa chereko, ngoma lipo uwanjanii Mwali na mideko, kama nimetoka ngomani Aii yuko wapi mamie mwali Aje anibebe mgongoni Amuite daddy mwali waje Wayarudi ya msondondo Bibi anacheka, zawadi kaleta Na kitenge na mkeka Na kibunda cha pesa (Aah aah aah) Habari ziende kwa ma ex Penzi waliodhulumu Tena nimepata tetesi Mmoja ataka kunywa sumu Kisaa jamani kisaa Nikauliza kisaa, kisa leo naolewa Naolewa, naolewa mie (ooh sheba) Naolewa, naolewa mie Sina sina makosa (mtoto wa mwenzio) Sina sina makosa (utajiua) Sina sina makosa (mtoto wa mwenzio) Sina sina makosa (utajiua buree) Buree, buree