Shika uliposhikwa, ujingapo achia Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia Shika uliposhikwa, ujingapo achia Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia Maneno, maneno, maneno Hayashibishi mtu Maneno, maneno, maneno Vita yagombanisha watu Hizi ni salamu, nakupatia Subira Mi sichokuwepo, nitakuwa nasikia Hizi ni salamu, nakupatia Subira mama Mi sitokuwepo, nitakuwa nasikia Ooh Subira, nisikiize sana Uendapo mbilini kuna mawifi, ujichunge mama Ooh Subira, nisikiize sana Uendapo mbilini kuna mawifi, ujichunge mama Acha kusangalai (umpende mumeo) We acha kusangalai (umtunze mumeo) Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki) Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki) Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki) Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki) Maneno, maneno, maneno Hayashibishi mtu Maneno, maneno, maneno Vita yagombanisha watu Mambo ya zamani, tofauti na sasa mwenzangu Na siri za ndani, zitunze kifuani mwenzangu Mambo ya zamani, tofauti na sasa mwenzangu Na siri za ndani, zisiwafikie walimwengu Aa chunga mdomo unajidanganya Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya Shoga eh kumbuka wanaume siku hizi wachache Akienda bafuni, akienda kazini akuage shoga eh Aa chunga mdomo unajidanganya Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya Aa ah hiyo nafasi usiitake, uiache utachekwa wee Wenzio wamaliza soli kwa waganga waipate Aah chunga mdomo unajidanganya Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya Hehehe ya, maji ya ugali hayaonjwi mwenzangu eh We mwana, mwana, mwanangu eh, eehh Utaniacha hoi hoi hoi Hata nikikuona sauti sitoi Utaniacha hoi hoi hoi Hata nikikuona sauti sitoi Shoga eh kumbuka wanaume siku hizi wachache Akienda bafuni, akienda kazini akuage shoga eeh Aah chunga mdomo unajidanganya Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya We Shirko we, jamani we Shirko wewe Shughuli imeambatana na mvua hii babu Wanyama wanakula wima Chezea, ah haa, neno la kishujaa babu Vita vifanyike ila raisi nisiuwawe Aah chunga mdomo unajidanganya Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya Utaniacha hoi hoi hoi Hata nikikuona sauti sitoi Utaniacha hoi hoi hoi Hata nikikuona sauti sitoi