Unaweza ukaniona nacheka Ila moyo wangu umeficha mengi Maisha yamejawa na heka heka Kila hatua moja ni kigingi Kuna vitu vingine vinaumiza Kula yangu ni ya kudunduliza Kuna muda nahisi kukata tamaa Ila nakumbuka mama ananitazamaaa Zagala zagala, langu buku linatosha Pilau la masimango, sio siri linachosha Zagala zagala, langu buku linatosha Pilau la masimango, sio siri linachosha Kukata tamaa sijafunzwa Nami namuomba Muumba Kukata tamaa sijafunzwa Nami namuomba Muumba Ona maisha, maisha magumu Nikikumbuka mbali nilipotoka Mengi nyumbani, nyumbani majukumu Ndo yalofanya shule nikaiacha Namshukuru sana Mungu Aah aah, wangu Mungu Japo mtaani kuna majungu Aah aah, mengi majungu Wabaya walimwengu Wenye chuki na mie Ambao hawataki niendelee Langu zuri kwenu baya waja nyie Na sijui kwanini hawataki niendelee Kukata tamaa sijafunzwa Nami namuomba Muumba Kukata tamaa sijafunzwa Nami namuomba Muumba