Kwetu kitanda cha kamba Si godoro si shuka ni mkeka Kibanda chenyewe chavuja, aah Nyumba yenyewe ya kupanga Shule nako majanga Shati viraka, viraka Nikiangalia haya wazazi wangu Namwonea huruma baba Fundi mwenza, mbeba nzege Usawa umemkaba Inamuuma roho mama yangu Mwanawe anadhalilika Shule ni ada, mida bwada Nguo zimeraruka Mama pressure inapanda Dada naye mgonjwa sana Kaka naye kapagawa Yuko milembe Baba sukari imebamba Ndugu hawana msaada Sote tuko njia panda Yaani mawenge Mang'amu ng'amu Nadondosha chozi nakufuru Mungu Mang'amu ng'amu Shida kwangu ndo kimbilio Mang'amu ng'amu Hivi lini mimi nitapata nafuu Mang'amu ng'amu Ooh Mtaani naitwa Kayumba Mara muuza karanga Mara muokota machupa, aah Kila duka deni hatujalipa Vikoba nao watutafuta Yaani mchaka mchaka Ninawaza sana Lini tutapata na sisi? Ututoke umasikini Inamuuma roho mama yangu Mwanawe anadhalilika Shule ni ada, mida bwada Nguo zimeraruka Mama pressure inapanda Dada naye mgonjwa sana Kaka naye kapagawa Yuko milembe Baba sukari imebamba Ndugu hawana msaada Sote tuko njia panda Yaani mawenge Mang'amu ng'amu Nadondosha chozi nakufuru Mungu Mang'amu ng'amu Shida kwangu ndo kimbilio Mang'amu ng'amu Hivi lini mimi nitapata nafuu Mang'amu ng'amu Ooh