Aah Tanzania, iye iye Aah Tanzania, iye iye Aah Tanzania (selo beats) Katika kila jambo Unaloliona lapendeza Jua kuna watu walioumia (Kwa ajili hilo) aah (kwa ajili hilo) Katika kila jambo Unaloliona lavutia Jua kuna watu waliotaabikia (Kwa ajili hilo) aah (kwa ajili hilo) Ni kweli Tanzania kuna amani ya kutosha Hilo tunajivunia Yatupasa tuliombee jeshi letu la taifa Mola alotujalia Wanapambana kwa ajili yetu ooh Ili tuwe salama salama Wanahangaika usiku na mchana ooh Miili yao wametoa sadaka ooh Wanalala kwenye vumbi na matope Ili sisi tulale vitandani mwetu Tunatembelea magari ya dhamani sana Wanatembelea vifaru na malori Asubuhi Unaamshwa na alamu ya simu yako Wao wanaamshwa Kwa milio ya mabomu na risasi Wanatoa sadaka yao leo Kwa manufaa ya kesho yako Wameyatoa sadaka ya maisha yao Ili kutetea maisha yako Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu) Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu) Unavaa mkanja mzuri kiuoni mwako eeh Wanavaa mikanja ya risasi Ii Ii Ii Unakula chakula ukipendacho, kile ukitamanicho Wanakula wadudu na matunda porini (porini) Tunavaa kofia maridadi Na nzuri zenye kupendeza Wanavaa kofia ngumu Na nzito tena za chuma Sijutii kuzaliwa Tanzania (Aah) Najivunia mimi kuwa Tanzania (Aah) Wanapambana kwa ajili yetu ooh Ili tuwe salama salama Wanahangaika usiku na mchana ooh Miili yao wametoa sadaka ooh Asubuhi Unaamshwa na alamu ya simu yako Wao wanaamshwa Kwa milio ya mabomu na risasi Wanatoa sadaka yao leo Kwa manufaa ya kesho yako Wameyatoa sadaka ya maisha yao Ili kutetea maisha yako Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu) Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu) Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu) Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania) Nchi yetu (ooh Tanzania) Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu) Jeshi letu (mashujaa wetu)