Na Nusu

Harmonize

    Continues after the ad

    mwanamke ni mtu na nusu
    kukatishwa tamaa usiruhusu

    mwanamke ni mtu na nusu
    kurudishwa nyuma usiruhusu

    na kama mwanaume ndo kichwa, cha familia
    basi mwanamke ndo shingo, na kiwiliwili

    amani ya mume aliye bora inatengenezwa na mke, anapoianza siku

    Continues after the ad

    hata furaha ya mume aliye bora inakamilishwa na mke, ifikapo usiku

    yeeh si ujinga kukubali matokeo ooh
    na sio suala la kupinga wanatuzidi upeo ooh
    ingekuwa hiari yangu mimi ningewapa kila cheo ooh
    muaadilifu kama mama yangu sijamuona mpaka leo ooh

    samia suluhu ni mtu na nusu
    mboni mpaye mpango ni mtu na nusu
    mariam mwinyi ni mtu na nusu
    mary majaliwa ni mtu na nusu
    dkt tulia ni mtu na nusu
    anna makinda ni mtu na nusu
    bibi titi ni mtu na nusu
    sophia kawawa ni mtu na nusu

    pata kucha litazama na lifike kiama
    hutomwona kama mama mama
    mwanamke ni kiumbe jasiri
    mama ndie mungu was pili
    ile miezi sita ni siri
    baba asingeweza hata miwili

    hata uwe tajiri tajiri kamwe huwezi kuwa na mama wawili wawili
    mume ataoa wawili
    mwanamke hawezi kuwa na wawili fikiri

    si ujinga kukubali matokeo ooh
    na sio suala la kupinga wanatuzidi upeo ooh
    ingekuwa hiari yangu mimi ningewapa kila cheo ooh
    muaadilifu kama mama konde sijamuona mpaka leo ooh

    maria nyerere ni mtu na nusu
    bi fatuma karume ni mtu na nusu
    sitti mwinyi ni mtu na nusu
    mama anna mkapa ni mtu na nusu
    salma kikwete ni mtu na nusu
    janeth magufuli ni mtu na nusu
    getrude mongela ni mtu na nusu
    bi mwenda ni mtu na nusu
    bi kidude ni mtu na nusu
    mama khadija kopa ni mtu na nusu

    Song details

    Composition: Harmonize

    Did you see an error?

    Enviar revisão