Sawa

Ibraah

    Continúa después del anuncio

    It's Bonga
    (Oh nah, nah, nah, nah, nah aah)

    Asante Mungu Baba uliye mwema
    Nimeiona siku nyingine ya furaha
    Hali sio haba sio njema
    Wa kuniponya nipate hata chembe ya furaha

    Maana wazazi wananitegemea
    Na ninakaribia mi kuitwa Baba
    Nami ndunguzo waloegemea
    Sina kitu nimechalala nimevava

    Uniepushe mabaya dunia
    Yasijenikumba
    Napiga goti kwa uchungu nalia
    Ni nusuru muumba

    Katu nisikate tamaa
    Niende kusaka tonge
    Nipate ama nishinde njaa
    Moyoni upige konde, ni sawa eh

    Ni sawa, ni sawa
    Nami nitafika (ata nikikosa sawa)
    Ni sawa, ni sawa
    Nami mimi utanipa (ah ridhiki we ndo unayegawa)

    Continúa después del anuncio

    Sawa, ni sawa
    Nami nitafika (mwanadamu hawezi panga)
    Ni sawa, ni sawa
    Nami mimi utanipa (sitozuguka kwa waganga)

    Natapa tapa elimu sina
    Mi kusoma sijasoma
    Nami nasaka nijenge heshima
    Mi nakoma ju wananichoma

    Ni wewe pekee ndo naye jua
    Ah mbele yangu na nyuma yangu
    Mie mpweke naomba dua
    Ah Baba fungua ridhiki zangu

    Nashukuru Baba, pumzi unayonipa
    Maisha naendelea
    Ila kingine Baba, nadhalilika
    Huu mzigo unanielemea

    Baba niwewe Baba (ni wewe)
    Niwe ndo msaada (ni wewe)
    Ni wewe, ni wewe
    Baba ni wewe

    Uniepushe mabaya dunia
    Yasijenikumba
    Napiga goti kwa uchungu nalia
    Ni nusuru muumba

    Katu sikate tamaa
    Niende kusaka tonge
    Nipate ama nishinde njaa
    Moyoni upige konde

    Ni sawa, ni sawa
    Nami nitafika (ata nikikosa sawa)
    Ni sawa, ni sawa
    Nami mimi utanipa (ah ridhiki we ndo unayegawa)

    Sawa, ni sawa
    Nami nitafika (mwanadamu hawezi panga)
    Ni sawa, ni sawa
    Nami mimi utanipa (sitozuguka kwa waganga)

    Información de la canción

    Composición:

    ¿Los datos están equivocados?

    Enviar revisión

    Canciones relacionadas