Sawa (feat. Kigoto)

Masauti

    Continues after the ad

    Sasa kila kitu doro
    Tumevumilia kwa maisha tumetusua
    Tulivyokula kiporo
    Nilifikiria tunda watalichukua

    Hakuna tena sorrow
    Ni muda wa kujivunia na kutulia
    Shopping twende Comoro
    Na unachofikiria nitakununulia

    Maisha yetu tamu yaani tende
    Sina sababu yaani bora nikupende
    Wewe ni kichwa mimi ni pembe
    Kama penzi nitakupa tamu usiende

    Ya habibi
    Ni wewe umenivumilia
    Sina budi
    Kukuwa nawe beiby

    Ulinishika nikashikilia, tukapenda
    Hawajui tulipoanzia, wanasengenya
    Mahaba we wanijulia, unazo tekenya
    Unapotaka tutaishia, daima kwenda

    Ooh beiby beiby na wala usione ghari
    Kwa hiyo maisha tunayokaa
    Ooh beiby beiby ukitaka pia magari
    Ukitaka juu tunapaa

    Continues after the ad

    Kila kitu sawa (sawa)
    Usijali mama kila siku uko na mimi
    Yaani sawa (sawa)
    Unachokipenda utakipata hapa mjini

    Nasema sawa (sawa)
    Tumetoka mbali sitakuendea pembeni
    Nasema sawa (sawa)
    Yaani sawa (sawa)

    Mi napenda unavyonukia
    Urembo wako wee wavutia
    Macho yako ukiniangalia
    Moyo wangu unatulia

    Kisura mi nagharamika mwenyewe
    Kwanini nisiwe na wewe
    Ka ni wakufura, tumeteseka wenyewe
    Waache wasituelewe

    Inshallah Mola tumuombe
    Akuondolee
    Maisha mema tuendelee
    Nyuma tusiregee

    Ya habibi
    Ni wewe umenivumilia
    Sina budi
    Kukuwa nawe beiby

    Ulinishika nikashikilia, tukapenda
    Hawajui tulipoanzia, wanasengenya
    Ni mahaba we wanijulia, unazo tekenya
    Unapotaka tutaishia, daima kwenda

    Dunia ilinifunza
    Ila wewe ukatulia
    Sasa nakutunza
    Na maisha twaurahia

    Kila kitu sawa (sawa)
    Usijali mama kila siku uko na mimi
    Yaani sawa (sawa)
    Unachokipenda utakipata hapa mjini

    Nasema sawa (sawa)
    Tumetoka mbali sitakuendea pembeni
    Nasema sawa (sawa)
    Yaani sawa (sawa)

    Song details

    Composition:

    Did you see an error?

    Enviar revisão