Continúa después del anuncio

    Sifa kwa mola wangu maulana, kwa mengi aliofanya
    Hadi mi na we kukutana, kisura
    Sijapanga kudanganya, ntasema ukweli mama
    Kisa nakupenda sana, kisura
    Umesema wanipenda, ila maisha yangu maseke
    Michicha, milenda ndo menyu yangu, na ya kuku mateke
    Yaani chenga, kila siku kilio sa lini nicheke?
    Sina tenda, ugali buguruni, mboga temeke
    Nafurahi umeniridhia niwe na wewe kimwali
    Maisha yangu mitihani isoisha maswali
    Ukifika nyumbani vumilia maana hali sio swali
    Asubuhi mchana pakavu, jioni ndo kula futali

    Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
    Viwalo vyetu, ukifua kumbuka kuvilinda
    Huku kwetu, muda wowote mateja wanatinga
    Hamahm
    Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi

    Bado, mi bado, mi bado
    Ndo kwanza nimepanga
    Bado, iyee, mi bado
    Sina hata kiwanja
    Bado, iyee, mi bado
    Kulipa kodi majanga
    Bado, mimi bado, mi bado ooh ooh

    Continúa después del anuncio

    Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro
    Ghetto namkeka tu hakuna kitanda, shuka wala godoro
    Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
    Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya comoro
    Ila nimeshakupa, nimeshakupa mtima mtima
    Ukija kususa, utanizika mzima mzima
    Nimeshakupa eh, nimeshakupa mtima mtima
    Ukija kususa ah, utanizika mzima mzima

    Tena, huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
    Viwalo vyetu, ukifua kumbuka kuvilinda
    Huku kwetu, muda wowote mateja wanatinga
    Hamahm
    Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi

    Bado, mi bado, mi bado (eh eh)
    Ndo kwanza nimepanga (eh eh)
    Bado, iyee, mi bado
    Sina hata kiwanja
    Bado, mie, mi bado
    Kulipa kodi majanga
    Bado, mimi bado, mi bado
    Suala la nyumba na gari mimi

    Bado, mi bado, mi bado
    (Haki ya mungu bado, yaani shuka bado)
    Ndo kwanza nimepanga
    Bado, iyee, mi bado
    Sina hata kiwanja (eh eh)
    Bado, iyee, mi bado (eh eh)
    Kulipa kodi majanga (oh uh uh)
    Bado, mimi bado, mi bado (iyee iyee)

    Información de la canción

    Composición: Rayvanny

    ¿Los datos están equivocados?

    Enviar revisión

    Canciones relacionadas