Cifra Club

Unaibiwa

Rayvanny

Aún no tenemos los acordes de esta canción.

Ayolizer

Usidate na njonjo za mapenzi
Vicheko bandia usoni kudeka kumbe Ana pretend
Maufundi toka Tanga na Zenji
Vionjo mitego unase ashike pochi umwage chenji

Anakuchanganya kiunoni shanga
Marashi kama uko peponi
Mtoto sauti kinanda
Ya kumtoa chatu pangoni
Ukishatafuna karanga
Hutaki hata aende sokoni
Anakuchuna mafaranga
Unabaki na vumbi mfukoni

Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi
Baby me I like that
Nakukupamba kwenye simu
Video Snapchat
Kumbe hana maana hadi mangi
Anamwita sweetheart
Kisa anakesha gym
Kutafuta six packs

Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa

Kuna kina Rose Visosa
Wale wapenda Verosa
Ukipita na shati na moka
Lazima watashoboka
Wakiomba lift, ogopa
Miguu dashboard vishoka
Mchunguze cheni, goroka
Nywele na pochi kakopa, eh

Usije kuyavamia yasije yakakutesa
Hawachelewagi kukimbia
Kuna wenzako wanalia
Walizani mapenzi pesa
Kwenye suruali vibamia

Hata ukimuonga Ferrari
Hatokuona rijali
Wakati chumbani we beki
Ukifunga moja tu chali
Atakamatwa na mangangali vijana machachali
Hawachagui sehemu ya vita uvunguni na juu ya dali

Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi
Baby me I like that
Nakukupamba kwenye simu
Video Snapchat
Kumbe hana maana hadi mangi
Anamwita sweetheart
Kisa anakesha gym
Kutafuta six packs

Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa

Unadhani niwapekeako
Kumbe wengine wameshaweka kambi
Kakupendea macho
Wapo wengine kawapendea rangi
Ye ni gari la dampo
Hachagui taka dereva mpe ganji
Wakubadili sample
Akila mihogo karoti hazipandi

Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa
Unaibiwa

Otros videos de esta canción
    0 visualizaciones

    Afinación de los acordes

    Afinador en línea

    Ops (: Contenido disponible solo en portugués.
    OK