Hayeye!
Nimesota, sina wera
Juzi nilikopa nilipe mama mboga
Hawajui, hawata amini
Juu mi ni mwana mziki na mambo yangu iko fiti
Na huko instagrama, wanadhani nimeosa
Sababu waliona nikikula na Obama
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia
Hayeye!
Chakula githeri chemsha na avocado
Na nina deni ya soo mbili ya mama Wambo
Sasa nasaka fare anagalau nifike show
Lakini jana si nilikua kwa TV
Na juzi pia nilikua kwa gazeti
Mambo yangu yanafaa kua fiti
Huko instagrama, wanadhani niko poa
Sababu waliona, ile poster ya Koroga
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia
Sio yote yang’aayo ni dhahabu
Watu huficha masaibu kwa tabasamu
Basi sote tuwe wakarimu
Sababu yote yang’aayo si dhahabu
Wengi ni mastar kwa vile wanavyo vaa
Lakini utashangaa, vile wanavyokaa
Wengi hujifanya mambo yao yako sawa
Lakini utashangaa, ni mengi haya ya dunia