Mashujaa Wetu

YPrince

    Continúa después del anuncio

    Aah Tanzania, iye iye
    Aah Tanzania, iye iye
    Aah Tanzania (selo beats)

    Katika kila jambo
    Unaloliona lapendeza
    Jua kuna watu walioumia
    (Kwa ajili hilo) aah (kwa ajili hilo)

    Katika kila jambo
    Unaloliona lavutia
    Jua kuna watu waliotaabikia
    (Kwa ajili hilo) aah (kwa ajili hilo)

    Ni kweli Tanzania kuna amani ya kutosha
    Hilo tunajivunia
    Yatupasa tuliombee jeshi letu la taifa
    Mola alotujalia

    Wanapambana kwa ajili yetu ooh
    Ili tuwe salama salama
    Wanahangaika usiku na mchana ooh
    Miili yao wametoa sadaka ooh

    Wanalala kwenye vumbi na matope
    Ili sisi tulale vitandani mwetu
    Tunatembelea magari ya dhamani sana
    Wanatembelea vifaru na malori

    Asubuhi
    Unaamshwa na alamu ya simu yako
    Wao wanaamshwa
    Kwa milio ya mabomu na risasi

    Continúa después del anuncio

    Wanatoa sadaka yao leo
    Kwa manufaa ya kesho yako
    Wameyatoa sadaka ya maisha yao
    Ili kutetea maisha yako

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Unavaa mkanja mzuri kiuoni mwako eeh
    Wanavaa mikanja ya risasi Ii Ii Ii
    Unakula chakula ukipendacho, kile ukitamanicho
    Wanakula wadudu na matunda porini (porini)

    Tunavaa kofia maridadi
    Na nzuri zenye kupendeza
    Wanavaa kofia ngumu
    Na nzito tena za chuma

    Sijutii kuzaliwa Tanzania
    (Aah)
    Najivunia mimi kuwa Tanzania
    (Aah)

    Wanapambana kwa ajili yetu ooh
    Ili tuwe salama salama
    Wanahangaika usiku na mchana ooh
    Miili yao wametoa sadaka ooh

    Asubuhi
    Unaamshwa na alamu ya simu yako
    Wao wanaamshwa
    Kwa milio ya mabomu na risasi

    Wanatoa sadaka yao leo
    Kwa manufaa ya kesho yako
    Wameyatoa sadaka ya maisha yao
    Ili kutetea maisha yako

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Twaiombea nchi yetu (ooh Tanzania)
    Nchi yetu (ooh Tanzania)
    Twaiombea jeshi letu (mashujaa wetu)
    Jeshi letu (mashujaa wetu)

    Información de la canción

    Composición:

    ¿Los datos están equivocados?

    Enviar revisión