Kwaru

Zuchu

    Continúa después del anuncio

    Iyoo lizer
    Aah ah aah

    Ah
    Roho ingekua na macho ungejionea
    Moyo haufanyi kificho ukigotea
    Mimi kipi nisonacho ungeongea
    Mwili wangu rochorocho nanyong’onyea
    Chungu nilichopika
    Wamepakua wenzangu
    Huruma napukutishwa
    Wamechukua tonge langu
    Na kitabu chetu cha mapenzi
    Kurasa umeichanachana
    Hazisomeki tena tenzi
    Zimepoteza maana

    Mpofu moyo wangu
    Ulishindwa ona
    Hukuandikwa wakwangu
    Limenikaba nalitema

    Continúa después del anuncio

    Kwaru kwakwaru kwaru
    Kachukua kisoda Ana ukwangua
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Moyo wangu unaumia
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Ah! Ye kwa nguvu Ana ukwarua
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Jamani moyo wangu
    Unaumia

    Eh
    Langu tatizo
    Nachunda najimaliza
    Mi nakesha kumuwaza
    Naweweseka lake jina (ooh jina)
    Oh! Basi kwa unyonge
    Najikaza niache kulia
    Mana kwake bahati sina (ooh sina)
    Maumivu ameipora furaha yangu
    Ooh amekwenda nayo
    Na zangu mbivu zimeniozea
    Mmh hasara kwangu
    Ooh oh! Yatajwisha nayoo

    Mpofu moyo wangu
    Ulishindwa ona
    Hukuandikwa wakwangu
    Limenikaba nalitema

    Kwaru kwakwaru kwaru
    Kachukua kisoda Ana ukwangua
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Moyo wangu unaumia
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Ah! Ye kwa nguvu Ana ukwarua
    Kwaru kwakwaru kwaru
    Jamani moyo wangu
    Unaumia

    Información de la canción

    Composición:

    ¿Los datos están equivocados?

    Enviar revisión

    Canciones relacionadas