Cifra Club

Ndoto Ya Mchana

Leteipa the King

Aún no tenemos los acordes de esta canción.

Niliskia tufununu, Kwamba ulipata mwingine
Anayekupenda zaidi ya mimi, mtafunga ndoa pengine
Yetu ilikuwa shadow, mapenzi yenu yamekolea
Lazima huwa Anakupa, vitu sikuwa nakupea
Ndoto zako zote, ulizoniambia
Naona kama kweli sasa zinatimia
Na Sina chochote, cha kukuambia
Ila nakonda Kweli nikikufikiria

Sura yako umbo lako jamani eeh
Busu na mahaba chumbani maami
Mawaidha yako nikiwa matatani eeh
Nikikumbuka najiona hayawani maami

Nawatakia mema (nawatakia mema)
Nawatakia mema (nawatakia mema)
Nawatakia mema (nawatakia mema)
Basi kwaheri kwaheri kwaheri Mami (ndoto yangu ya Mchana)

Ingawa inaniuma, niko na furaha moyoni
Kuona kwamba umepata, vyote ulivyokuwa unatamani
Naomba nipate mwaliko, wa harusi nije Nile wali
Nipige picha na wadau, nikupe zawadi kama zamani
Alafu ntapeform, kama beshte yako, kale kawimbo nilikuimbia shambani
Na nitakuinform, tunza mume wako, Japo kuna vitu zenye ninatamani

Ingawa ningependa, ungekuwa wangu pekee (nawatakia mema)
Ingawa moyoni umeniachia kidonda (nawatakia mema)
Namwomba Mungu, anipatie mwingine Kama wewe (nawatakia mema)
Hivo kwaheri kwaheri kwaheri kwaheri mama (ndoto yangu ya Mchana)
Lakini ninaomba, unifanyie favour Moja (nawatakia mema)
Ukijifungua kama ni wa kiume, mpe jina laangu (nawatakia mema)
Na kama ni wa kike mpe jina la mama yangu (nawatakia mema)
Basi kwaherii (ndoto yangu ya Mchana)

Otros videos de esta canción
    0 visualizaciones

    Afinación de los acordes

    Afinador en línea

    Ops (: Contenido disponible solo en portugués.
    OK