Cifra Club

Nilinde

Kusah

Aún no tenemos los acordes de esta canción.

Mmh mmh, ooh ooh
Aiiehh eeh eeh
(Gachi beats)

Nawaza na sipati majibu
Mbona haya ni majaribu
Au Baba unanijaribu
Maana mi sipati jawabu ila

Labda langu ni dogo
Kuna makubwa ya wengine
Yaani kwa hiki kidogo
Nisikufuru na mengine

Mmh kuna muda mi nakataga tamaa
Najiuliza lini nitasimama
Mbona mimi ni wa kushika tama
Mmh

Si unajua maadui ni wengi
Kuna muda mi nawazaga mengi
Maana mambo yananoga
Labda wananiroga

Maana napiga zoga
Hadi napata uoga
Maana mambo yananoga
Labda wananiroga

Maana napiga zoga
Hadi napata uoga

Oooh Baba nilinde, Baba nilinde
Niepushe nikinge, simama nilinde
Basi Baba nilinde, Baba nilinde
Niepushe nikinge, simama nilinde

Mmh, mmh, mmh
Ayee ayee ayeee

Kuna muda nalia
Nikifikiria naona hili ni dogo
Maana kuna wasio na hatia
Na wamepotea wangali wadogo

Ila mimi napumua
Na pumzi silipii sasa nitake nini?
Ati nisipate matatizo milele
Kwani mi ni nani?

Si unajua maadui ni wengi
Kuna muda mi nawazaga mengi
Maana mambo yananoga
Labda wananiroga

Maana napiga zoga
Hadi napata uoga
Maana mambo yananoga
Labda wananiroga

Maana napiga zoga
Hadi napata uoga

Ooh Baba nilinde, Baba nilinde
Niepushe nikinge, simama nilinde
Basi Baba nilinde, Baba nilinde
Niepushe nikinge, simama nilinde

Baba nilinde, Baba nilinde
Baba nilinde, Baba nilinde
Baba nilinde, Baba nilinde
Baba nilinde, Baba nilinde

Otros videos de esta canción
    0 visualizaciones

    Afinación de los acordes

    Afinador en línea

    Ops (: Contenido disponible solo en portugués.
    OK