Eti Lava utaoa lini, mbona unazingua?
Wazuri wengi mjini wezi wanachukua
We kutwa ubishoo, nywele kuchange mitindo
Wanakuona wafoo, kila siku uko single
Moyo wa kupenda sina ya nini nijipe homa
Si huyu ni mwana Stamina rafiki yake Roma
Si unajua ndoa majaliwa
Nasubiria apange Maulana
Atanitunukia bado naula ujana
Ujana maji ya moto, utakuunguza (nitakuunguza)
We pita peku mpoto tutakuuguza
Kwanza kuolewa raha
Oh nah nah wili wili
Ona mume wangu hii spa
Atumiliki wawili wili
Umenikumbusha kule Insta udaku
Wanasema mume umekwara
Ati umefuata hela
Ukakubali kuolewa mitara
Hutanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini?
Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela
Kwanza naona mapenzi, faida hayana
Bora niwe bachela eh
Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana
Bora niwe bachela!
Dada Darleen acha kunichachafya
Uliza kilomkuta Dangote
Sijui kangombana na Tanasha
Ametu-unfollow wote
Mapenzi ya siku hizi
Shemeji Lokole mwongoza umbea
Mkigombana tu kashatizi
Insta nzima yameshaenea
Ndio maana nimetulia
Navuta pumzi staki kwenda mbio
Mambo ya kujifanya hodari eti mjuzi
Ujuzi huo kwio
Tukiachana na yote
Mimi bado sikuungi mkono
Wasafi wote
Mnaonekana mnapenda ngono (duu)
Hutanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini?
Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela
Kwanza naona mapenzi, faida hayana
Bora niwe bachela eh
Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana
Mabachela piga kelele (wee)
Piga kelele moja (wee)
Kelele mbili (wee wee)
Piga kelele tatu (wee)
Wenye wapenzi piga kelele (wee)
Walio oa (wee)
Tulio olewa je? (Wee)
(Abby Daddy)