Shika uliposhikwa, ujingapo achia
Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia
Shika uliposhikwa, ujingapo achia
Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia
Maneno, maneno, maneno
Hayashibishi mtu
Maneno, maneno, maneno
Vita yagombanisha watu
Hizi ni salamu, nakupatia Subira
Mi sichokuwepo, nitakuwa nasikia
Hizi ni salamu, nakupatia Subira mama
Mi sitokuwepo, nitakuwa nasikia
Ooh Subira, nisikiize sana
Uendapo mbilini kuna mawifi, ujichunge mama
Ooh Subira, nisikiize sana
Uendapo mbilini kuna mawifi, ujichunge mama
Acha kusangalai (umpende mumeo)
We acha kusangalai (umtunze mumeo)
Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki)
Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki)
Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki)
Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki)
Maneno, maneno, maneno
Hayashibishi mtu
Maneno, maneno, maneno
Vita yagombanisha watu
Mambo ya zamani, tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani, zitunze kifuani mwenzangu
Mambo ya zamani, tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani, zisiwafikie walimwengu
Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Shoga eh kumbuka wanaume siku hizi wachache
Akienda bafuni, akienda kazini akuage shoga eh
Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Aa ah hiyo nafasi usiitake, uiache utachekwa wee
Wenzio wamaliza soli kwa waganga waipate
Aah chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Hehehe ya, maji ya ugali hayaonjwi mwenzangu eh
We mwana, mwana, mwanangu eh, eehh
Utaniacha hoi hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi
Shoga eh kumbuka wanaume siku hizi wachache
Akienda bafuni, akienda kazini akuage shoga eeh
Aah chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
We Shirko we, jamani we Shirko wewe
Shughuli imeambatana na mvua hii babu
Wanyama wanakula wima
Chezea, ah haa, neno la kishujaa babu
Vita vifanyike ila raisi nisiuwawe
Aah chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Utaniacha hoi hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi