Nderemoo, na vifijo si mayowe
Te amo, furaha yangu kupendwa na wewe
Maneno wasemayo na yapuza ujue
Sikurushi roho nikuache uumie
Na sina sifa ya kuku
Kila da ni nipakue mie
Wala lopo ya kasubu
Ya watu niyahadithie
Upole wangu tausi
Vigengeni hunikuti
Na sina huba la nuksi
Nakshi zangu ni marashi
Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea
Sawa
Kusemwa nishazoea
Haya
Mwenzako nishazoea
Mi sitovaa vimini vya mpasuo kwetu mwiko
Natinga baibui mwilini na videra vya baikoko
Tena najitia uturi viyasmini vya mtoko
Nikupeleke nyumbani
Kisiwa cha karafuu
Tukale madoriani
Shoki shoki za udambu
Jioni twende forodhani
Tukale upepo mwanana
Chaza mchukue mwambani
Na iwe zawadi ya mama
Upole wangu tausi
Vigengeni hunikuti
Na sina huba la nuksi
Nakshi zangu ni marashi
Sawa
Kusemwa nishazoea (aah ahh ah)
Haya
Mwenzako nishazoea (nishazoea mie)
Sawa
Kusemwa nishazoea (ooh ooh oh oh)
Haya
Mwenzako nishazoea (nishazoea miee eeh)