Ninavyo kuangalia wapendeza
Waufanya moyo wangu udunde
Sijawahi kuyahisi haya yote
Umenipa mapenzi tele tele
Tumehusiana kwa muda mfupi
Sikudhani nitakutana na we
Kila siku pambazuko la mapenzi
Wewe malkia mimi mfalme
Ni wewe, kipenzi cha maisha
Kilelele cha raha sitafika
Si ndwele yale yaliyopita
Nataka tuwe pamoja milele
Kwa loli mlungu wanirasimia
Wanineka mndu mcha unikunde
Ngelo ihi namfunyira chawucha
Kwa gose aga wanibonyera
Ni wewe, kipenzi cha maisha
Kilelele cha raha sitafika
Si ndwele yale yaliyopita
Nataka tuwe pamoja milele
Dikaie kwa lukundo kwa kala
Matuku ge lola gaida
Ni wewe, kipenzi cha maisha
Kilelele cha raha sitafika
Si ndwele yale yaliyopita
Nataka tuwe pamoja milele