Cifra Club

Kijuso (feat. Rayvanny)

Queen Darleen

Aún no tenemos los acordes de esta canción.

Eyoo Laizer
Wasafi Records

Unaringa kitu gani, we mwenyewe ujisute
Afadhali hata nyani, sio we mwanamke!
Hupendezi asilani, sio unyoe, usuke
Nilifata kitu gani? Umefanya nijute!

Mi nakuona punguwani, na usikurupuke
Kwanza naongea na nani? Naomba nikumbushe
Mi nawe hatuendani, jipandishe jishushe!
Usinipande kichwani, namba yangu ifute

Hizo dharau, mwana mvyoro papu
Naona unasahau nyuzi zako nilikapu

Nimepanda dau, mkataba nimekata
Tena nyang'au, ndo ukome kunifata

Unaringa una nini? Kijuso!
Vijimeno kama jini, Gaucho!

Kwani nawe una nini? Kituko!
Usio na kazi mjini, popo!

Punguza kelele
Acha kelele mama

Punguza kelele baba
Acha kelele bwana

Eti nawe unavimba, perfume tu mtihani!
Kwanza shirt ulovaa umeazima kwa nanii
Wanifata kapuku, utanipa nini?
Nilikuacha, leo kimekuwasha nini?

Funga bakuli mbele yangu we mshamba
Nakujua vizuri toka unavaa mabwanga
Kati unanuka moshi, huna hata ishu!
Kwenye pochi wanja na tishu

Unapenda ganda la ndizi, kuteleza
Wakati kupambana mpaka mchuzi wa pweza!
Dume zima tantara tantara
Instagram ina hue
Wakati kwenu kula, kulala, huchangii hata kitunguu

Hizo dharau, mwana mvyoro papu
Naona unasahau nyuzi zako nilikapu

Nimepanda dau, mkataba nimekata
Tena nyang'au, ndo ukome kunifata

Unaringa una nini? Kijuso!
Vijimeno kama jini, Gaucho!

Kwani nawe una nini? Kituko!
Usio na kazi mjini, popo!

Punguza kelele
Acha kelele mama

Punguza kelele baba
Acha kelele bwana

Otros videos de esta canción
    0 visualizaciones

    Afinación de los acordes

    Afinador en línea

    Ops (: Contenido disponible solo en portugués.
    OK