Unaweza ukaniona nacheka
Ila moyo wangu umeficha mengi
Maisha yamejawa na heka heka
Kila hatua moja ni kigingi
Kuna vitu vingine vinaumiza
Kula yangu ni ya kudunduliza
Kuna muda nahisi kukata tamaa
Ila nakumbuka mama ananitazamaaa
Zagala zagala, langu buku linatosha
Pilau la masimango, sio siri linachosha
Zagala zagala, langu buku linatosha
Pilau la masimango, sio siri linachosha
Kukata tamaa sijafunzwa
Nami namuomba Muumba
Kukata tamaa sijafunzwa
Nami namuomba Muumba
Ona maisha, maisha magumu
Nikikumbuka mbali nilipotoka
Mengi nyumbani, nyumbani majukumu
Ndo yalofanya shule nikaiacha
Namshukuru sana Mungu
Aah aah, wangu Mungu
Japo mtaani kuna majungu
Aah aah, mengi majungu
Wabaya walimwengu
Wenye chuki na mie
Ambao hawataki niendelee
Langu zuri kwenu baya waja nyie
Na sijui kwanini hawataki niendelee
Kukata tamaa sijafunzwa
Nami namuomba Muumba
Kukata tamaa sijafunzwa
Nami namuomba Muumba